Mithali 12

Mke mwenye tabia nzuri ni taji ya mumewe, bali aaibishaye ni kama uozo katika mifupa ya mumewe.

Proverbs 12:4 (UKJV) A virtuous woman is a crown to her husband: but she that makes ashamed is as rottenness in his bones.

2Mtu mwema hupata kibali kutoka kwa Bwana, bali Bwana humhukumu mwenye hila.

3Mtu hathibitiki kutokana na uovu, bali mwenye haki hataondolewa.

4Mke mwenye tabia nzuri ni taji ya mumewe, bali aaibishaye ni kama uozo katika mifupa ya mumewe.

5Mipango ya mtu mwadilifu ni ya haki, bali ushauri wa mwovu ni udanganyifu.

6Maneno ya waovu huotea kumwaga damu, bali maneno ya waadilifu huwaokoa.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.