12Kilichotarajiwa kikikawia kuja moyo huugua, bali tumaini lililotimizwa ni mti wa uzima.
13Yeye anayedharau mafundisho anajiletea maangamizi, bali yeye anayeheshimu agizo hupewa tuzo.
14Mafundisho ya mwenye busara ni chemchemi ya uzima, ili kumwepusha mtu na mitego ya mauti.
15Ufahamu mzuri hupata upendeleo, bali njia ya asiye mwaminifu ni ngumu.
16Kila mwenye busara hutenda kwa maarifa, bali mpumbavu hudhihirisha upumbavu wake.