4Mvivu hutamani sana na hapati kitu, bali nafsi ya mwenye bidii hutoshelezwa kikamilifu.
5Mwenye haki huchukia uongo, bali waovu huleta aibu na fedheha.
6Haki humlinda mtu mwadilifu, bali uovu humwangusha mwenye dhambi.
7Mtu mmoja hujifanya tajiri, kumbe hana chochote; mwingine hujifanya maskini, kumbe ana utajiri mwingi.
8Utajiri wa mtu waweza kukomboa maisha yake, bali mtu maskini hasikii kitisho.