5Mwenye haki huchukia uongo, bali waovu huleta aibu na fedheha.
6Haki humlinda mtu mwadilifu, bali uovu humwangusha mwenye dhambi.
7Mtu mmoja hujifanya tajiri, kumbe hana chochote; mwingine hujifanya maskini, kumbe ana utajiri mwingi.
8Utajiri wa mtu waweza kukomboa maisha yake, bali mtu maskini hasikii kitisho.
9Nuru ya mwenye haki hungʼaa sana, bali taa ya mwovu itazimwa.