7Mtu mmoja hujifanya tajiri, kumbe hana chochote; mwingine hujifanya maskini, kumbe ana utajiri mwingi.
8Utajiri wa mtu waweza kukomboa maisha yake, bali mtu maskini hasikii kitisho.
9Nuru ya mwenye haki hungʼaa sana, bali taa ya mwovu itazimwa.
10Kiburi huzalisha magomvi tu, bali hekima hupatikana kwa wale wanaozingatia ushauri.
11Fedha isiyo ya halali hupungua, bali yeye akusanyaye fedha kidogo kidogo huongezeka.