9Bwana huchukia sana njia ya waovu, bali huwapenda wale wafuatao haki.
10Adhabu kali humngoja yeye aachaye njia; yeye achukiaye maonyo atakufa.
11Mauti na Uharibifu viko wazi mbele za Bwana: je, si zaidi sana mioyo ya wanadamu!
12Mwenye mzaha huchukia maonyo; hatataka shauri kwa mwenye hekima.
13Moyo wenye furaha hufanya uso uchangamke, bali maumivu ya moyoni huponda roho.