Mithali 15

Mwenye mzaha huchukia maonyo; hatataka shauri kwa mwenye hekima.

Proverbs 15:12 (UKJV) A scorner loves not one that reproves him: neither will he go unto the wise.

10Adhabu kali humngoja yeye aachaye njia; yeye achukiaye maonyo atakufa.

11Mauti na Uharibifu viko wazi mbele za Bwana: je, si zaidi sana mioyo ya wanadamu!

12Mwenye mzaha huchukia maonyo; hatataka shauri kwa mwenye hekima.

13Moyo wenye furaha hufanya uso uchangamke, bali maumivu ya moyoni huponda roho.

14Moyo wa mwenye ufahamu hutafuta maarifa, bali kinywa cha mpumbavu hujilisha upumbavu.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.