15Siku zote za wanaoonewa ni za taabu, bali moyo mchangamfu una karamu ya kudumu.
16Afadhali kuwa na kidogo pamoja na kumcha Bwana, kuliko mali nyingi pamoja na ghasia.
17Afadhali chakula cha mboga mahali palipo na upendo kuliko nyama ya ndama iliyonona pamoja na chuki.
18Mtu mwepesi wa hasira huchochea ugomvi, bali mtu mvumilivu hutuliza ugomvi.
19Njia ya mvivu imezibwa na miiba, bali njia ya mwenye haki ni barabara kuu.