25Bwana hubomoa nyumba ya mtu mwenye kiburi, bali huilinda mipaka ya mjane isiguswe.
26Bwana huchukia sana mawazo ya mwovu, bali mawazo ya wale walio safi humfurahisha yeye.
27Mtu mwenye tamaa huletea jamaa yake taabu, bali yeye achukiaye rushwa ataishi.
28Moyo wa mwenye haki hupima majibu yake, bali kinywa cha mwovu hufoka ubaya.
29Bwana yuko mbali na waovu, bali husikia maombi ya wenye haki.