Mithali 15

Bwana huchukia sana mawazo ya mwovu, bali mawazo ya wale walio safi humfurahisha yeye.

Proverbs 15:26 (UKJV) The thoughts of the wicked are an abomination to the LORD: but the words of the pure are pleasant words.

24Mapito ya uzima huelekea juu kwa ajili ya wenye hekima kumwepusha asiende chini kaburini.

25Bwana hubomoa nyumba ya mtu mwenye kiburi, bali huilinda mipaka ya mjane isiguswe.

26Bwana huchukia sana mawazo ya mwovu, bali mawazo ya wale walio safi humfurahisha yeye.

27Mtu mwenye tamaa huletea jamaa yake taabu, bali yeye achukiaye rushwa ataishi.

28Moyo wa mwenye haki hupima majibu yake, bali kinywa cha mwovu hufoka ubaya.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.