1Jawabu la upole hugeuza ghadhabu, bali neno liumizalo huchochea hasira.
2Ulimi wa mwenye hekima husifu maarifa, bali kinywa cha mpumbavu hufoka upumbavu.
3Macho ya Bwana yako kila mahali, yakiwaangalia waovu na wema.
4Ulimi uletao uponyaji ni mti wa uzima, bali ulimi udanganyao huponda roho.
5Mpumbavu hubeza maonyo ya baba yake, bali yeyote akubaliye maonyo huonyesha busara.