28Moyo wa mwenye haki hupima majibu yake, bali kinywa cha mwovu hufoka ubaya.
29Bwana yuko mbali na waovu, bali husikia maombi ya wenye haki.
30Mtazamo wa tabasamu huleta furaha moyoni, nazo habari njema huipa mifupa afya.
31Yeye asikilizaye maonyo yatoayo uzima atakuwa miongoni mwa wenye hekima.
32Yeye anayedharau maonyo hujidharau mwenyewe, bali yeyote anayekubali maonyo hupata ufahamu.