27Mtu mbaya kabisa hupanga mabaya, maneno yake ni kama moto uunguzao.
28Mtu mpotovu huchochea ugomvi, nayo maongezi ya upuzi hutenganisha marafiki wa karibu.
29Mtu mkali humvuta jirani yake na kumwongoza katika mapito yale mabaya.
30Yeye akonyezaye kwa jicho lake anapanga upotovu; naye akazaye midomo yake amenuia mabaya.
31Mvi ni taji ya utukufu; hupatikana kwa maisha ya uadilifu.