15Moyo wa mwenye ufahamu hujipatia maarifa, masikio ya mwenye hekima huyatafuta maarifa.
16Zawadi humfungulia njia mtoaji, nayo humleta mbele ya wakuu.
17Yeye aliye wa kwanza kuleta mashtaka huonekana sahihi, hadi mwingine ajitokezapo na kumuuliza maswali.
18Kupiga kura hukomesha mashindano na kutenganisha wapinzani wakuu wanaopingana.
19Ndugu aliyechukizwa ni mgumu kuridhika kuliko mji uliozungushiwa ngome, nayo mabishano ni kama malango ya ngome yenye makomeo.