14“Haifai, haifai!” asema mnunuzi, kisha huondoka akijisifia ununuzi wake.
15Dhahabu kunayo, na marijani kwa wingi, lakini midomo inenayo maarifa ni kito cha thamani kilicho adimu.
16Chukua vazi la yule awekaye dhamana kwa ajili ya mgeni; lishikilie iwe dhamana kama anafanya hivyo kwa ajili ya mwanamke mpotovu.
17Chakula kilichopatikana kwa hila ni kitamu kwa mwanadamu, bali huishia na kinywa kilichojaa changarawe.
18Fanya mipango kwa kutafuta mashauri, ukipigana vita, tafuta maelekezo.