18Fanya mipango kwa kutafuta mashauri, ukipigana vita, tafuta maelekezo.
19Maneno ya kusengenya husababisha kutokuaminika, kwa hiyo mwepuke mtu anayezungumza kupita kiasi.
20Ikiwa mtu atamlaani baba yake au mama yake, taa yake itazimwa katika giza nene.
21Urithi upatikanao haraka mwanzoni, hautabarikiwa mwishoni.
22Usiseme, “Nitakulipiza kwa ajili ya kosa hili!” Mngojee Bwana, naye atakuokoa.