Mithali 21

Mtu mwovu hutamani sana ubaya, jirani yake hapati huruma kutoka kwake.

Proverbs 21:10 (UKJV) The soul of the wicked desires evil: his neighbour finds no favour in his eyes.

8Njia ya mwenye hatia ni ya upotovu, bali tabia ya mtu asiye na hatia ni nyofu.

9Ni afadhali kuishi pembeni mwa paa la nyumba, kuliko kuishi nyumba moja na mke mgomvi.

10Mtu mwovu hutamani sana ubaya, jirani yake hapati huruma kutoka kwake.

11Wakati mwenye mzaha ameadhibiwa, mjinga hupata hekima; wakati mtu mwenye hekima afundishwapo, hupata maarifa.

12Mwenye Haki huyajua yanayotendeka katika nyumba za waovu, naye atawaangamiza waovu.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.