1Moyo wa mfalme uko katika mkono wa Bwana; huuongoza kama mkondo wa maji, popote apendapo.
2Njia zote za mwanadamu huonekana sawa kwake, bali Bwana huupima moyo.
3Kufanya yaliyo sawa na haki inakubalika zaidi kwa Bwana kuliko dhabihu.
4Macho ya kudharau na moyo wa kiburi, ambavyo ni taa ya waovu, vyote ni dhambi!
5Mipango ya mwenye bidii huelekeza kwenye faida, kama vile kwa hakika pupa huelekeza kwenye umaskini.