6Mfundishe mtoto njia impasayo kuiendea, naye hataiacha hata akiwa mzee.
7Matajiri huwatawala maskini naye akopaye ni mtumwa wa akopeshaye.
8Yeye aupandaye uovu huvuna taabu, nayo fimbo ya ghadhabu yake itaangamizwa.
9Mtu mkarimu yeye mwenyewe atabarikiwa kwa kuwa hushiriki chakula chake na maskini.
10Mfukuze mwenye dhihaka, na mvutano utatoweka; ugomvi na matukano vitakoma.