8Utatapika kile kidogo ulichokula, nawe utakuwa umepoteza bure maneno yako ya kumsifu.
9Usizungumze na mpumbavu, kwa maana atadhihaki hekima ya maneno yako.
10Usisogeze jiwe la mpaka wa zamani wala kunyemelea kwenye mashamba ya yatima,
11kwa kuwa Mtetezi wao ni mwenye nguvu, atalichukua shauri lao dhidi yako.
12Elekeza moyo wako kwenye mafundisho na masikio yako kwenye maneno ya maarifa.