31Usiukodolee macho mvinyo wakati ukiwa mwekundu, wakati unapometameta kwenye bilauri, wakati ushukapo taratibu!
32Mwishowe huuma kama nyoka na kutia sumu yake kama nyoka mwenye sumu.
33Macho yako yataona mambo mageni na moyo wako kuwazia mambo yaliyopotoka.
34Utakuwa kama alalaye katikati ya bahari, alalaye juu ya kamba ya merikebu.
35Utasema, “Wamenipiga lakini sikuumia! Wamenichapa, lakini sisikii! Nitaamka lini ili nikanywe tena?”