1Usiwaonee wivu watu waovu, usitamani ushirika nao;
2kwa maana mioyo yao hupanga mambo ya jeuri, nayo midomo yao husema juu ya kuleta madhara.
3Kwa hekima nyumba hujengwa, nayo kwa njia ya ufahamu huimarishwa
4kwa njia ya maarifa vyumba vyake hujazwa vitu vya thamani na vya kupendeza.