30Nilipita karibu na shamba la mvivu, karibu na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili,
31miiba ilikuwa imeota kila mahali, ardhi ilikuwa imefunikwa na magugu, na ukuta wa mawe ulikuwa umebomoka.
32Nikatafakari moyoni mwangu lile nililoliona, nami nikajifunza somo kutokana na niliyoyaona:
33Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, bado kukunja mikono kidogo upate kupumzika:
34hivyo umaskini utakuja juu yako kama mnyangʼanyi, na kupungukiwa kutakujia kama mtu mwenye silaha.