20Kuzimu na Uharibifu havishibi kadhalika macho ya mwanadamu.
21Kalibu ni kwa ajili ya fedha na tanuru kwa ajili ya dhahabu, bali mtu hupimwa kwa sifa azipokeazo.
22Hata ukimtwanga mpumbavu kwenye kinu, ukimtwanga kama nafaka kwa mchi, hutauondoa upumbavu wake.
23Hakikisha kuwa unajua hali ya makundi yako ya kondoo na mbuzi, angalia kwa bidii ngʼombe zako.
24Kwa kuwa utajiri haudumu milele, nayo taji haidumu vizazi vyote.