8Hii itakuletea afya mwilini mwako, na mafuta kwenye mifupa yako.
9Mheshimu Bwana kwa mali zako na kwa malimbuko ya mazao yako yote;
10ndipo ghala zako zitakapojaa hadi kufurika, viriba vyako vitafurika kwa mvinyo mpya.
11Mwanangu, usiidharau adhabu ya Bwana na usichukie kukaripiwa naye,
12kwa sababu Bwana huwaadibisha wale awapendao, kama vile baba afanyavyo kwa mwana apendezwaye naye.