6katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyoosha mapito yako.
7Usiwe mwenye hekima machoni pako mwenyewe; mche Bwana ukajiepushe na uovu.
8Hii itakuletea afya mwilini mwako, na mafuta kwenye mifupa yako.
9Mheshimu Bwana kwa mali zako na kwa malimbuko ya mazao yako yote;
10ndipo ghala zako zitakapojaa hadi kufurika, viriba vyako vitafurika kwa mvinyo mpya.