4Ndipo utapata kibali na jina zuri mbele za Mungu na mwanadamu.
5Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote wala usizitegemee akili zako mwenyewe;
6katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyoosha mapito yako.
7Usiwe mwenye hekima machoni pako mwenyewe; mche Bwana ukajiepushe na uovu.
8Hii itakuletea afya mwilini mwako, na mafuta kwenye mifupa yako.