13Heri mtu yule aonaye hekima, mtu yule apataye ufahamu,
14kwa maana hekima ana faida kuliko fedha na mapato yake ni bora kuliko ya dhahabu safi.
15Hekima ana thamani kuliko marijani; hakuna chochote unachokitamani kinachoweza kulinganishwa naye.
16Maisha marefu yako katika mkono wake wa kuume; katika mkono wake wa kushoto kuna utajiri na heshima.
17Njia zake zinapendeza, mapito yake yote ni amani.