23Kisha utaenda katika njia yako salama, wala mguu wako hautajikwaa;
24ulalapo, hautaogopa; ulalapo usingizi wako utakuwa mtamu.
25Usiogope maafa ya ghafula au maangamizi yanayowapata waovu,
26kwa kuwa Bwana atakuwa tumaini lako na kuepusha mguu wako kunaswa katika mtego.
27Usizuie wema kwa wale wanaostahili ikiwa katika uwezo wako kutenda.