22ndipo vitakapokuwa uzima nafsini mwako na pambo la neema shingoni mwako.
23Kisha utaenda katika njia yako salama, wala mguu wako hautajikwaa;
24ulalapo, hautaogopa; ulalapo usingizi wako utakuwa mtamu.
25Usiogope maafa ya ghafula au maangamizi yanayowapata waovu,
26kwa kuwa Bwana atakuwa tumaini lako na kuepusha mguu wako kunaswa katika mtego.