20kwa maarifa yake vilindi viligawanywa, nayo mawingu yanadondosha umande.
21Mwanangu, hifadhi maamuzi mema na busara, usiache vitoke machoni pako;
22ndipo vitakapokuwa uzima nafsini mwako na pambo la neema shingoni mwako.
23Kisha utaenda katika njia yako salama, wala mguu wako hautajikwaa;
24ulalapo, hautaogopa; ulalapo usingizi wako utakuwa mtamu.