26kwa kuwa Bwana atakuwa tumaini lako na kuepusha mguu wako kunaswa katika mtego.
27Usizuie wema kwa wale wanaostahili ikiwa katika uwezo wako kutenda.
28Usimwambie jirani yako, “Njoo baadaye, nitakupa kesho”: wakati wewe unacho kitu kile karibu nawe.
29Usifanye hila ya kumdhuru jirani yako, ambaye anaishi karibu na wewe akikuamini.
30Usimshtaki mtu bila sababu, wakati hajakutenda dhara lolote.