11“Wako watu wale ambao huwalaani baba zao na wala hawawabariki mama zao;
12wale ambao ni safi machoni pao wenyewe kumbe hawakuoshwa uchafu wao;
13wale ambao daima macho yao ni ya kiburi, ambao kutazama kwao ni kwa dharau;
14wale ambao meno yao ni panga na ambao mataya yao yamewekwa visu kuwaangamiza maskini katika nchi, na wahitaji kutoka miongoni mwa wanadamu.
15“Mruba anao binti wawili waliao, ‘Nipe! Nipe!’ “Kuna vitu vitatu visivyotosheka kamwe, naam, viko vinne visivyosema, ‘Yatosha!’: