24“Vitu vinne duniani vilivyo vidogo, lakini vina akili nyingi sana:
25Mchwa ni viumbe wenye nguvu ndogo, hata hivyo hujiwekea akiba ya chakula chao wakati wa kiangazi.
26Pelele ni viumbe vyenye uwezo mdogo hata hivyo hujitengenezea nyumba zao kwenye miamba.
27Nzige hawana mfalme, hata hivyo huenda pamoja vikosi vikosi.
28Mjusi anaweza kushikwa kwa mkono, hata hivyo huonekana katika majumba ya kifalme.