10Mke mwenye sifa nzuri, ni nani awezaye kumpata? Yeye ni wa thamani sana kuliko marijani.
11Mume wake anamwamini kikamilifu wala hakosi kitu chochote cha thamani.
12Humtendea mumewe mema, wala si mabaya, siku zote za maisha yake.
13Huchagua sufu na kitani naye hufanya kazi kwa mikono yenye bidii.
14Yeye ni kama meli za biashara akileta chakula chake kutoka mbali.