4“Ee Lemueli, haifai wafalme, haifai wafalme kunywa mvinyo, haifai watawala kutamani sana kileo,
5wasije wakanywa na kusahau vile sheria inavyoamuru na kuwanyima haki zao wote walioonewa.
6Wape kileo wale wanaoangamia, mvinyo wale walio na uchungu,
7Wanywe na kusahau umaskini wao na wasikumbuke taabu yao tena.
8“Sema kwa ajili ya wale wasioweza kujisemea, kwa ajili ya haki za wote walioachwa ukiwa.