4baba alinifundisha akisema, “Yashike maneno yangu yote kwa moyo wako wote; yashike maagizo yangu na wewe utaishi.
5Pata hekima, pata ufahamu; usiyasahau maneno yangu wala usiyaache.
6Usimwache hekima naye atakuweka salama; mpende, naye atakulinda.
7Hekima ni bora kuliko vitu vyote; kwa hiyo jipe hekima. Hata ikikugharimu vyote ulivyo navyo, pata ufahamu.
8Mstahi, naye atakukweza; mkumbatie, naye atakuheshimu.