6Usimwache hekima naye atakuweka salama; mpende, naye atakulinda.
7Hekima ni bora kuliko vitu vyote; kwa hiyo jipe hekima. Hata ikikugharimu vyote ulivyo navyo, pata ufahamu.
8Mstahi, naye atakukweza; mkumbatie, naye atakuheshimu.
9Atakuvika shada la neema kichwani mwako na kukupa taji ya utukufu.”
10Sikiliza mwanangu, kubali ninachokuambia, nayo miaka ya maisha yako itakuwa mingi.