8Mstahi, naye atakukweza; mkumbatie, naye atakuheshimu.
9Atakuvika shada la neema kichwani mwako na kukupa taji ya utukufu.”
10Sikiliza mwanangu, kubali ninachokuambia, nayo miaka ya maisha yako itakuwa mingi.
11Ninakuongoza katika njia ya hekima na kukuongoza katika mapito yaliyonyooka.
12Utembeapo, hatua zako hazitazuiliwa; ukimbiapo, hutajikwaa.