10Sikiliza mwanangu, kubali ninachokuambia, nayo miaka ya maisha yako itakuwa mingi.
11Ninakuongoza katika njia ya hekima na kukuongoza katika mapito yaliyonyooka.
12Utembeapo, hatua zako hazitazuiliwa; ukimbiapo, hutajikwaa.
13Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; mshike, maana yeye ni uzima wako.
14Usiuweke mguu wako katika njia ya waovu wala usitembee katika njia ya watu wabaya.