Mithali 6

kama umetegwa na ulichosema, umenaswa kwa maneno ya kinywa chako,

Proverbs 6:2 (UKJV) You are snared with the words of your mouth, you are taken with the words of your mouth.

1Mwanangu, kama umekuwa mdhamini wa jirani yako, ikiwa umeshika mikono kwa kuweka ahadi kwa ajili ya mwingine,

2kama umetegwa na ulichosema, umenaswa kwa maneno ya kinywa chako,

3basi fanya hivi mwanangu, ili ujiweke huru, kwa kuwa umeanguka mikononi mwa jirani yako: Nenda ukajinyenyekeshe kwake; msihi jirani yako!

4Usiruhusu usingizi machoni pako, usiruhusu kope zako zisinzie.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.