2kama umetegwa na ulichosema, umenaswa kwa maneno ya kinywa chako,
3basi fanya hivi mwanangu, ili ujiweke huru, kwa kuwa umeanguka mikononi mwa jirani yako: Nenda ukajinyenyekeshe kwake; msihi jirani yako!
4Usiruhusu usingizi machoni pako, usiruhusu kope zako zisinzie.
5Jiweke huru, kama swala mkononi mwa mwindaji, kama ndege kutoka kwenye mtego wa mwindaji.
6Ewe mvivu, mwendee mchwa; zitafakari njia zake ukapate hekima!