19shahidi wa uongo ambaye humwaga uongo, na mtu ambaye huchochea fitina kati ya ndugu.
20Mwanangu, zishike amri za baba yako, wala usiyaache mafundisho ya mama yako.
21Yafunge katika moyo wako daima, yakaze kuizunguka shingo yako.
22Wakati utembeapo, yatakuongoza; wakati ulalapo, yatakulinda; wakati uamkapo, yatazungumza nawe.
23Kwa maana amri hizi ni taa, mafundisho haya ni mwanga na maonyo ya maadili ni njia ya uzima,