23Kwa maana amri hizi ni taa, mafundisho haya ni mwanga na maonyo ya maadili ni njia ya uzima,
24yakikulinda na mwanamke aliyepotoka, kutokana na maneno laini ya mwanamke aliyepotoka.
25Moyo wako usitamani uzuri wake wala macho yake yasikuteke,
26kwa maana kahaba atakufanya uwe maskini, hata ukose kipande cha mkate, naye mwanamke mzinzi huwinda maisha yako hasa.
27Je, mtu aweza kuchotea moto kwenye paja lake bila nguo zake kuungua?