18Hili na liandikwe kwa ajili ya kizazi kijacho, ili taifa litakaloumbwa baadaye waweze kumsifu Bwana:
19“Bwana alitazama chini kutoka patakatifu pake palipo juu, kutoka mbinguni alitazama dunia,
20kusikiliza vilio vya uchungu vya wafungwa na kuwaweka huru wale waliohukumiwa kufa.”
21Kwa hiyo jina la Bwana latangazwa huko Sayuni na sifa zake katika Yerusalemu,
22wakati mataifa na falme zitakapokusanyika ili kumwabudu Bwana.