1Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Ee Bwana Mungu wangu, wewe ni mkuu sana, umejivika utukufu na enzi.
2Amejifunika katika nuru kama vile kwa vazi, amezitandaza mbingu kama hema
3na kuziweka nguzo za orofa yake juu ya maji. Huyafanya mawingu kuwa gari lake, na hupanda kwenye mbawa za upepo.
4Huzifanya pepo kuwa wajumbe wake, miali ya moto watumishi wake.