14Akawatoa katika giza na huzuni kuu na akavunja minyororo yao.
15Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma, na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu,
16kwa kuwa yeye huvunja malango ya shaba na kukata mapingo ya chuma.
17Wengine wakawa wapumbavu kutokana na uasi wao, wakapata mateso kwa sababu ya uovu wao.
18Wakachukia kabisa vyakula vyote, wakakaribia malango ya mauti.