6Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao, naye akawaokoa kutoka taabu yao.
7Akawaongoza kwa njia iliyo sawa hadi mji ambao wangeweza kuishi.
8Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma, na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu,
9kwa maana yeye humtosheleza mwenye kiu, na kumshibisha mwenye njaa kwa vitu vyema.
10Wengine walikaa gizani na katika huzuni kuu, wafungwa wakiteseka katika minyororo,