12Asiwepo mtu yeyote wa kumtendea mema wala wa kuwahurumia yatima wake.
13Uzao wake na ukatiliwe mbali, majina yao yafutike katika kizazi kifuatacho.
14Maovu ya baba zake na yakumbukwe mbele za Bwana, dhambi ya mama yake isifutwe kamwe.
15Dhambi zao na zibaki daima mbele za Bwana, ili apate kukatilia mbali kumbukumbu lao duniani.
16Kwa maana kamwe hakuweza kutenda wema, bali alimfukuza mnyonge na mhitaji, aliwafanyia jeuri wahitaji na waliovunjika moyo.