Zaburi 116

Kamba za mauti zilinizunguka, maumivu makuu ya kuzimu yalinipata, nikalemewa na taabu na huzuni.

Psalm 116:3 (UKJV) The sorrows of death compassed me, and the pains of hell got hold upon me: I found trouble and sorrow.

1Ninampenda Bwana kwa maana amesikia sauti yangu; amesikia kilio changu ili anihurumie.

2Kwa sababu amenitegea sikio lake, nitamwita siku zote za maisha yangu.

3Kamba za mauti zilinizunguka, maumivu makuu ya kuzimu yalinipata, nikalemewa na taabu na huzuni.

4Ndipo nikaliitia jina la Bwana: “Ee Bwana, niokoe!”

5Bwana ni mwenye neema na haki, Mungu wetu ni mwingi wa huruma.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.